Jumatatu, 9 Mei 2016

Nauli za Mabasi yaendayo haraka ziko hapa, siku mbili bure


Baada ya Kampuni ya UDA-RT kuwasilisha maombi ya nauli zitakazotumika kwa mabasi yaendayo haraka kwa Mamlaka ya udhibiti usafiri wa nchi kavu na majini (SUMATRA) May 09 206 SUMATRA imetangaza nauli hizo.
SUMATRA imesema kuwa njia ya pembezoni (Freeder Route) nauli ya mtu mzima ni 400 na mwanafunzi 200 na njia kuu (Trunk Route) ni 650 na mwanafunzi 200 na kwa abiria atakayetumia kusafiri njia kuu (Freeder Route) na kuendelea na safari kwa njia ya pembezoni nauli yake itakuwa ni 800 na mwanafunzi 200. 
Huduma hiyo itatolewa kuanzia kesho bure kwa wananchi kwa siku mbili na May 12 2016 zitaanza kutozwa nauli zilizotajwa
.

Baada ya kuwasainisha mikataba ya kubaini watumishi hewa, RC Makonda kafanya maamuzi haya



Mei 2 2016 Mkuu wa mkoa Dar es salaam Paul Makonda aliwaapisha wakuu wa idara na maofisa utumishi wote lengo likiwa ni kuwataka kila mtumishi kuwabainisha watumishi wao hewa katika idara zao na atakayebainika kutoa taarifa zisizo sahihi mkataba umfunge mwenyewe.
Leo May 09 2016 katika uchunguzi wa awamu ya tatu wamekuja na ripoti ya watumishi hewa 39 walioisababishia Serikali hasara ya BILIONI 3.6.
Paul Makonda amemsimamisha kazi afisa utumishi wa Manispaa ya Ilala, Francis Kilawe kwa kutowagundua watumishi hewa 11 ambao walikuwa hawajulikani wapo idara gani
.